Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- vyanzo vya kuaminika vimeripoti siku ya Jumatatu kwamba vikosi hivyo vya uhandisi vimeanza kazi hiyo mapema asubuhi na tayari minara kadhaa imejengwa kwenye maeneo ya juu ya mlima huo, takriban kilomita 9 ndani ya ardhi ya Iraq. Minara hiyo inatumika kwa ajili ya mawasiliano ya kijeshi na kuhakikisha uhusiano kati ya kambi na maeneo ya wanajeshi katika eneo hilo.
Chanzo hicho kimeongeza kuwa jeshi la Uturuki lina mtandao mkubwa wa miundombinu ya mawasiliano ya waya na isiyo na waya ndani ya Iraq na limeanzisha zaidi ya vituo 70 vya kijeshi nchini humo. Baadhi ya vituo hivyo ni kambi kubwa, ambapo muhimu zaidi ipo pembezoni mwa mji wa Bashiqa.
Kimeeleza pia kwamba wanajeshi wa Uturuki wanatumia hali ya utulivu katika baadhi ya maeneo kuendeleza uwepo wao, hususan katika sekta ya mawasiliano kupitia minara mirefu.
Your Comment